Gauni lililotengenezwa kwa mikate 500 lilivyowashangaza wengi katika tuzo za filamu Afrika

Muda wa kusoma: Dakika 7

Mara nyingi hafla hii huelezewa kama usiku mkubwa zaidi barani Afrika katika filamu na mitindo ya mavazi.

Watu maarufu, watengenezaji filamu na wabunifu walihudhuria toleo la 12 la tuzo za Africa Magic Viewers' Choice Awards nchini Nigeria wakiwa wamevalia mavazi ya kuvutia yenye mikia mirefu, gauni za kisanii, vitambaa vinavyong'aa, na miundo ya maonesho ya kipekee ambayo iligeuza tena hafla hiyo kutoka kuwa sherehe ya tuzo kuwa tamasha la mitindo.

Fainali hiyo ilifanyika katika Eko Hotel and Suites mjini Lagos. Sherehe hiyo ya kila mwaka huadhimisha mafanikio katika filamu za Afrika, vipindi vya televisheni na simulizi za kidijitali, huku pia ikiwa mojawapo ya maonesho makubwa ya kitamaduni barani Afrika ambapo nyota hushindana sio tu kwa tuzo, bali pia kwa nani amevaa vizuri zaidi.

Zulia la mwaka huu liliegemea kabisa kwenye uoneshaji wa mitindo ya kupitiliza na ya kuvutia sana.

Baadhi ya watu maarufu walionekana wakitembea wakiwa na timu zao za wasaidizi waliobeba mavazi makubwa kupita kiasi kupitia umati wa wapiga picha na mashabiki waliokuwa wakipiga kelele.

Haya hapa ni baadhi ya matukio na uonekano uliovutia zaidi na kuzungumziwa sana usiku huo.

Zulia jekundu linageuka kuwa duka la kuoka mikate

Queen Mercy Atang alifika akiwa amevaa mojawapo ya mavazi yaliyovutia zaidi usiku huo, gauni lililotengenezwa kwa zaidi ya mikate 500, kwa mujibu wa yeye mwenyewe.

Akiwa amezungukwa na wasichana wawili waliobeba sahani za mikate na wasaidizi kadhaa waliomsaidia kubeba mavazi hayo makubwa kupitia zulia jekundu, Atang alionekana akiwa na ugumu wa kutembea kwa uhuru.

Akizungumza na BBC, alisema kuwa mavazi hayo yalibuniwa kutangaza biashara yake ya uokaji mikate na akasisitiza kuwa Muonekano huo ulikuwa mkakati wa makusudi wa masoko badala ya kutafuta tu usikivu wa watu.

"Ni sehemu gani bora zaidi ya kutangaza biashara yangu kuliko Africa Magic Viewers' Choice Awards?" alisema.

Gauni hilo lilibuniwa na mbunifu mashuhuri Toyin Lawani wa Tiannah's Empire, ambaye alitoa maoni kwenye Instagram akisema anaanzisha mtindo wa "kila mtu vaa biashara yako".

Muonekano huo uligeuka mara moja kuwa mojawapo ya mada kubwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii usiku huo.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao walipongeza ubunifu huo, wakisema ni "ufafanuzi halisi wa kubeba biashara yako kichwani."

Hata hivyo, si kila mtu alifurahishwa. Wengine waliona kuwa ni upotevu wa chakula, hoja ambayo nyota huyo wa reality TV aliipinga.

Nana Akua Addo anawasili akiwa amevaa gauni linalofanana na kanisa kubwa

Nyota wa mitindo kutoka Ghana, Nana Akua Addo, alizidi kuimarisha sifa yake ya kuleta mavazi ya kuvutia na ya kisanii kwenye Africa Magic Viewers' Choice Awards kwa kuvaa gauni la fedha lenye muundo wa usanifu wa kipekee lililoongozwa na Cologne Cathedral nchini Ujerumani.

Mavazi hayo yaliyokuwa na muundo mgumu sana yalijumuisha maelezo yaliyopakwa kwa mkono yanayofanana na madirisha ya kioo, sehemu zilizotengenezwa kwa umbo la kanisa, na vifaa vya mapambo vya rangi ya fedha vinavyolingana, huku timu yake wakisaidia kubeba baadhi ya sehemu za gauni hilo kupitia zulia jekundu.

Mbunifu wake, Abasswoman, aliiambia BBC kwamba mchakato wa kubuni ulianza Novemba 2025 na ulikamilika siku mbili tu kabla ya sherehe hiyo.

Kwa mujibu wa timu yake, mtindo huo uliongozwa na muundo wa kihistoria wa kanisa hilo maarufu, huku gauni likilenga kuonesha ukuu wa usanifu pamoja na ustadi wa hali ya juu wa ubunifu wa mitindo.

Uche Montana embraces fire and rebirth

Uche Montana alifika akiwa amevalia vazi la kuvutia la rangi nyekundu na dhahabu lililopambwa kwa manyoya, ambalo alilielezea kuwa linaashiria "moto" na "kufufuka kwa ndege aina ya phoenix."

Akiwa amevaa pia mapambo ya mawe mekundu mikononi mwake, mwigizaji huyo aliiambia BBC kuwa muonekano huo ulikuwa umekuwa ukibuniwa tangu mwanzo wa mwaka.

Ingawa alikataa kutaja kiasi halisi cha fedha kilichotumika, alisema kuwa alitumia "kiasi kikubwa" kufanikisha nguo hiyo, akiongeza kuwa moja ya dhana potofu kuhusu mitindo ya nyota hao ni kwamba huvalishwa bure kabisa na makampuni ya mitindo.

"Aina hii ya mavazi inahitaji kazi nyingi za kifedha na kiakili," alisema.

Muonekano wake ulihitimisha usiku mkubwa kwa mwigizaji huyo, ambaye pia alipokea tuzo ya AMVCA Trailblazer Award, tuzo isiyo ya upigaji kura inayotambua vipaji vinavyochipukia na vinavyoleta athari kubwa katika tasnia ya filamu.

Bucci Franklin's emotional win for 'To Kill a Monkey'

Mbali na tamasha la mitindo, mojawapo ya matukio ya kugusa hisia usiku huo ilitokea pale mwigizaji Bucci Franklin aliposhinda tuzo ya Muigizaji Bora Msaidizi kwa nafasi yake ya "Oboz" katika filamu ya "To Kill a Monkey".

Franklin anacheza mhusika wa kiongozi wa genge la uhalifu wa mtandaoni mwenye sauti kubwa na uaminifu wa hali ya juu, ambaye tabia yake imejikita sana katika utambulisho wa mitaa ya Benin. Ili kujiandaa na nafasi hiyo, alisoma kuhusu wasanii wa mtandaoni wa Benin, muziki wao na pia undani wa lahaja, vipengele ambavyo watazamaji wengi walivipongeza kwa uhalisia wake.

Uigizaji huo uliwagusa sana watazamaji wengi, hasa katika eneo la Niger Delta nchini Nigeria, kutokana na jinsi mhusika huyo alivyoakisi utambulisho wa eneo hilo.

Akizungumza na BBC baada ya ushindi wake, Franklin alisema kuwa ingawa mhusika huyo hakuwa na uhusiano wowote na tabia yake halisi, alifurahi sana kukubali jukumu hilo.

Alitoa tuzo hiyo kwa heshima ya mama yake, ambaye alifariki siku saba kabla ya filamu hiyo kutolewa.

Filamu "To Kill a Monkey" pia ilishinda tuzo ya picha Bora ya Filamu.

Linda Ejiofor makes history with two big awards

Linda Ejiofor aliibuka kama mmoja wa washindi wakubwa wa usiku huo, akiweka historia katika tuzo za Africa Magic Viewers' Choice kwa kuwa mtu wa kwanza kushinda tuzo zote mbili: Muigizaji Bora Mkuu wa Kike kwa filamu "The Serpent's Gift" na Muigizaji Bora Msaidizi wa Kike kwa "The Herd".

Akizungumza baada ya ushindi wake, aliiambia BBC kuwa alitarajia kushinda angalau katika kipengele kimoja, lakini alisema mume wake alijaribu kumtuliza kabla ya hafla kwa kumwambia kwamba huenda akaondoka na tuzo zote mbili. Mwishowe, hilo lilitimia.

Ejiofor alitambua mchango wa familia yake alipokuwa akitafakari ushindi huo, akielezea kuwa ulikuwa wakati wenye hisia kali sana. Alisema mama yake alimsaidia sana katika matamshi ya lugha ya Igbo, akimsaidia kuboresha uzungumzaji wa lugha hiyo hadi alipojisikia kuwa na ujasiri wa kutosha kwa nafasi hiyo.

'My Father's Shadow' wins three awards

Filamu "My Father's Shadow" iliendelea na mfululizo wake wa kutambuliwa kimataifa, ikiwa miongoni mwa washindi wakubwa wa usiku huo kwa kushinda tuzo ya Filamu Bora (Best Movie), Muongozaji Bora (Best Director) na Uandishi Bora (Best Writing) katika Africa Magic Viewers' Choice Awards.

Filamu hiyo iliyoongozwa na Akinola Davies Jr ilizishinda kazi nyingine zilizokuwa zikishindania tuzo hizo, zikiwemo "The Herd", "The Serpent's Gift" na "Gingerrr".

Filamu hiyo inayohusu kumbukumbu za upendo wa baba, kutengana na majonzi, pia iliweka historia kwa kuwa filamu ya kwanza ya Nigeria kuchaguliwa rasmi katika tamasha maarufu la filamu la Cannes mwaka 2025. Ilioneshwa pia katika sinema nchini Nigeria na Uingereza.

Wakati huohuo, Uzor Arukwe alishinda tuzo ya Muigizaji Bora Mkuu wa Kiume kwa filamu "Colours of Fire", huku wakongwe wa tasnia, Sola Sobowale na Kanayo O. Kanayo, wakitunukiwa Tuzo za Heshima (Lifetime Achievement Awards).

Kanayo O. Kanayo alielezea mavazi yake kama "mchanganyiko wa muonekano wa mtu mwenye mamlaka, utajiri wa zamani (old money) na mtindo wa mafia ulioshonwa kwa ustadi."

Alivalishwa na kampuni ya mitindo Prinz Innovation, kwa lengo la kuakisi haiba yake ya uigizaji kwenye skrini kama mtu tajiri, mwenye ushawishi na mtindo wa hali ya juu.

Stan Nze, anayejulikana kwa uigizaji wake unaoakisi utamaduni wa Kabila la Igbo, alifika akiwa amevalia mavazi ya rangi nyeusi na akiwa amebeba ufagio wake a kipekee cha jadi kilichochongwa na kutengenezwa kwa ngozi ya farasi.

Nyota wa TV na muigizaji Tobi Bakre alileta taswira ya kifalme ya Kiyoruba kwenye zulia jekundu akiwa amevalia vazi la jadi la agbada lililobuniwa na Deji na Kola, akiwa pia amebeba fimbo ya shaba iliyotengenezwa kwa mtindo maalum.

Monica Friday alijipambanua katika zulia jekundu kwa kuvaa gauni la rangi ya zambarau lililopambwa na bendera za nchi saba, zikiwemo pia ya Iran.

Alielezea mavazi hayo kama heshima kwa "ulimwengu unaovuja damu" na pia kama wito wa amani duniani, akisisitiza kuwa uumbaji huo ulikuwa na ujumbe wa kisiasa na kibinadamu badala ya urembo tu.

Osas Ighodaro amekuwa akijulikana kwa kushinda tuzo ya "mavazi bora" katika Africa Magic Viewers' Choice Awards kwa miaka kadhaa, ingawa kipengele hicho kiliondolewa mwaka huu. Hata hivyo, mavazi yake kwenye zulia jekundu bado husubiriwa kwa hamu kubwa katika tasnia ya Nollywood.

Mwaka huu alivaa gauni la fedha lililobuniwa na Veekee James, lenye muundo wa korseti na sketi inayotiririka kwa ustadi, likipambwa kwa mamia ya mawe ya mapambo yaliyolifanya liang'ae kwa kuvutia sana.

Waumbaji wa maudhui ya kidijitali pia walitembea kwenye zulia jekundu wakimeta na kung'aa wakiwa wamevaa mavazi ya kiutamaduni na gauni za kisanii zilizo na miundo ya kuchongwa kwa ustadi.

Nyota wa TV, OJ Posharella alipamba zulia jekundu akiwa na utepe mkubwa uliokaa kichwani mwake, akivutia macho ya wengi.

Alionekana akiwa amevalia vazi la tabaka nyingi lenye rangi mbalimbali, ambalo alijibunia mwenyewe, na hivyo kuongeza msisimko na ubunifu wa kipekee katika tukio hilo.