Unajua ukubwa wa dola trilioni moja? Mifano 7 ya utajiri 'wa kufuru' wa Elon Musk

Chanzo cha picha, Getty Images
Mmiliki wa makampuni ya teknolojia ya SpaceX na Tesla, Elon Musk, anakaribia kuweka rekodi ya kuwa trilionea ambayo wa kwanza dunia kwa kufikia utajiri wa zaidi ya dola trilioni moja.
Kwa sasa Musk anamiliki hisa zenye thamani ya takribani dola bilioni 273 kupitia kampuni ya Tesla pekee. Lakini ikiwa thamani ya kampuni yake ya SpaceX itaendelea kupanda kama ambavyo wawekezaji wengi wanatarajia, utajiri wake unaweza kuongezeka kwa mamia ya mabilioni ya dola zaidi.
Umiliki wake kwa pamoja Tesla na SpaceX unaweza kufikisha thamani inayozidi dola trilioni 1.1. Hiyo ni sawa na dola bilioni 1,100 au dola milioni milioni 1.1.
Ni kiwango cha utajiri ambacho hakijawahi kufikiwa na mtu yeyote katika historia ya dunia. Lakini dola trilioni moja ni kiasi gani hasa? Huu ni mifano 7 kuonyesha ukubwa wa fedha hizo.
Lakini dola trilioni moja ni kiasi gani hasa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Dola trilioni moja ni sawa na dola bilioni 1,000, unaweza kuitumia miaka zaidi ya 5,000.
Njia ya pili ya kuelewa kiasi hicho ni kuigawanya kwa watu wote duniani. Kwa sasa idadi ya watu duniani inakadiriwa kufikia takribani bilioni 8.3. Kama Musk angamua na kugawa dola trilioni 1.1 kwa kila mtu duniani mpaka watoto, basi kila mtu angepata karibu dola 133.
Hiyo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania 350,000 kwa kila mtu au karibu shilingi za Kenya 17,000 kwa kila mtu. Kwa familia ya watu watano au 6, mgao huo ungefikia karibu shilingi milioni 2 za Tanzania au karibu shilingi 90,000 za Kenya.
Na kama kila mmoja angeamua kutumia shilingi 100,000 za Tanzania kwa siku, fedha hizo zingemtosha kwa zaidi ya siku tatu mfululizo bila kufanya kazi yoyote.
Hata hivyo, ukubwa wa dola trilioni moja unaonekana zaidi unapolinganishwa na matumizi ya serikali na uchumi wa nchi.
Bajeti za Tanzania, Kenya na Uganda kwa karibu miaka 14

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Bajeti ya Tanzania kwa mwaka uliopita wa fedha 2025/26 ilikuwa takribani shilingi trilioni 56, sawa na karibu dola bilioni 22.
Kwa dola trilioni 1.1 zinnaweza kutosha kufadhili bajeti nzima ya Tanzania kwa karibu miaka 50 mfululizo.
Kwa maneno mengine, mtu mwenye utajiri huo angeweza kugharamia elimu, afya, miundombinu, ulinzi na mishahara ya watumishi wa umma kwa karibu nusu karne.
Kwa upande wa Kenya, ambayo iliidhinisha bajeti ya takribani Ksh trilioni 4.6 kwa mwaka wa fedha uliopita, karibu dola bilioni 35, utajiri huo ungeweza kufadhili matumizi yote ya serikali kwa zaidi ya miaka 30.
Uganda, ambayo ilipitisha bajeti ya takribani dola bilioni 20 kwa mwaka, ingeweza kufadhiliwa kwa zaidi ya miaka 55 na kiasi hiki cha utajiri.
Hata ukiamua kuzichanganya bajeti za nchi zote hizi tatu za Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda kwa pamoja zinafikia karibu dola bilioni 77 kwa mwaka.
Dola trilioni 1.1 zingetosha kabisa kugharamia bajeti za nchi zote tatu kwa zaidi ya miaka 14 mfululizo.
Mataifa 20 tu duniani yatamzidi Musk kwa utajiri

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ni nchi chache sana duniani zenye uchumi unaozidi dola trilioni 1.1. Zinatajwa kuwa nchi 20 tu zenye uchumi unaozidi $1.1 trillion.
Kati ya nchi 195 zinazotambuliwa duniani zikiwemo 193 chini ya Umoja wa Mataifa zitakuwa na uchumi mdogo kuliko utajiri huo atakaoufikia Musk.
Barani Afrika hakuna taifa hata moja lenye uchumi unaofikia dola trilioni moja kwa sasa.
Hata nchi zenye uchumi mkubwa zaidi kama Afrika Kusini, Misri, Algeria, Nigeria, bado zitakuwa chini ya kiwango hicho cha utajiri.
Angeweza kununua Zanzibar mara ngapi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Hakuna takwimu rasmi kuhusu thamani ya Zanzibar au ya mali zote zilizopo katika majiji kama Dar es Salaam, Nairobi au Mombasa.
Lakini kama utajiri huo unaweza kununua mali katika jiji kama Houston, jiji la tatu kw aukubwa Marekani, unaweza kuona ingeweza kununua mali kiasi gani katika majiji makubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Tanga, Nairobi na Mombasa.
Kwa lugha rahisi, utajiri wa kiwango hicho ungeweza kununua sehemu kubwa ya mali za miji mingi mikubwa ya Afrika Mashariki na bado kubakiza mamia ya mabilioni ya dola kununua mikoa kama Tabora, Morogoro (Tanzania) na Kaunti za Garissa, Isiolo, Taita-Taveta, Kiambu na Machakos huko Kenya.
Lakini ni utajiri wa karatasi

Chanzo cha picha, Getty Images
Pamoja na ukubwa wake, ni muhimu kuelewa kuwa utajiri wa Musk hauko katika akaunti ya benki kama fedha taslimu.
Sehemu kubwa ya mali yake inatokana na thamani ya hisa zake katika kampuni mbalimbali. Ikiwa thamani ya hisa hizo itashuka, utajiri wake unaweza pia kupungua kwa kiwango kikubwa.
Hata hivyo, kama atafikia kiwango cha dola trilioni moja, Musk ataingia katika eneo jipya kabisa la utajiri ambalo halijawahi kufikiwa na mwanadamu yeyote katika historia ya dunia.
Makala hii imeandaliwa kupitia vyanzo mbalimbali na kwa kuboreshwa kwa msaada wa AI












